• A boat with beautiful sunset.
  • JKM GET TOGETHER
  • Amaizing sunrise moment

SHEREHE YA UZINDUZI WA TAWI LA UUGUZI CHINI YA MTAKATIFU AGATHA-19/05

Wanajumuiya wa mt Agatha wakiwa wanasikiliza kwa makini kinachoendele kwenye sherehe hiyo

Baba paroko na Mlezi wa JKM akiwashukuru wanajumuiya kwa Kufungua tawi rasmi na kuwapa pongezi za kumchagua Mt Agatha kuwa msimamizi wa tawi.Aliwaasa wanajumuiya wote Kuchagua wito mapema na kuusimamia kwa imani kama Mt somo alivyo onesha mfano mzuri

Baathi ya wageni waalikwa wakiwa wanatumbuizwa na bwana MC.Wageni hao walikuwa kutoka Jumuiya nyingine na Kwaya za JKM


wanajumuiya wakiwa wanakula chakula cha sherehe

wageni wakipata chochote



HISTORIA FUPI YA JUMUIYA

Tumsifu yesu kristo.
Ifuatayo ni historia fupi ya jumuiya.
Jumuiya ya Uuguzi ilianza rasmi mwaka 2008 mara tu baada ya kufunguliwa kwa Parokia ya Bikira Maria Salama ya wagonjwa Muhimbili wanaishi Jumuiya yetu ilifahamika kwa jina la jumuiya ya Wauguzi.
Baada ya Parokia kukua na kwa kutambua umuhimu wa Jumuiya katika parokia uongozi wa Jumuiya Katoliki Muhimbili (JKM) kwa kushirikiana na Kamati tendaji ya Parokia,ilipendekeza Jumuiya zote zipewe majina ya Watakatifu ambao pia watakuwa wasimamizi wa jumuiya hizo
Mnamo mwishoni mwa mwaka 2011,jumuiya zote zilipewa majina yaliyochaguliwa na wanajumuiya wenyewe.Majina haya yalianza kutumika mwanzoni mwa mwaka 2012.Sisi wanajumuiya wa tawi la Uuguzi tulioendekeza Jumuiya yetu iitwe Jumuiya ya Mt,Agatha ambaye kanisa limemuweka kuwa msimamizi wa Wauuguzi wote.
Na leo hii tar 19/5/2013 Jumuiya hii imesimikwa rasmi na baba Paroko Pd.F Mushi kwa hiyo tangu leo jukuiya hii itafahamika rasmi kwa jina la Jumuiya ya MT AGATHA

ilisomwa na mwenyekiti wa tawi.

SHARE ON:

Hello guys, I'm Tien Tran, a freelance web designer and Wordpress nerd. Sed ut perspiciatis unde omnis iste natus error sit voluptatem accusantium doloremque laudantium, totam rem aperiam, eaque ipsa quae.

1 comments:

  1. HONGERENI SANA NA MUNGU WA MAJESHI AWE NANYI DAIMA. www.jumuiyabmm.blogspot.com

    ReplyDelete