AGENDA ZA KIKAO CHA HALMASHAULI 6/07 Saa 2:00asbh-5:3asbh
JUMUIYA
KATOLIKI MUHIMBILI
KIKAO CHA HALMASHAURI
YA JKM, JUMAMOSI TRH 06/07/2013
saa2:00asbh – 5:30asbh
AGENDA ZA KIKAO
- MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI
2013/2014: Rejea pendekezo la bajeti lililoambatanishwa. Kikao kitajadili,
kurekebisha na kupitisha makadirio
hayo.( nakala za bajeti.zipo kwa wenyeviti wa matawi na viongozi jkm, ubao
wa matangazo ofisini, facebook na www.jkmmcc.blogspot)
- JKM GRAND FUND RAISING:
Bahasha na fomu kwa wakatoliki wote
wanaosoma MUHAS.
Fomu zitakuwa ndani ya kila bahasha
na tunapendekeza watu wapitishe fomu kwa ndugu na jamaa zao wakati wa likizo.
Hatulazimishi mtu kutembeza fomu, ia
kini walau kila fomu na bahasha yake irudi na kima cha chini ambacho
mapendekezo ni Tsh 10000 ( elfu kumi za kitanzania). Tunapendekeza watu watoe
zaidi ili kupata fedha ya kutosha kuendesha hadi mwaka 2015 au zaidi bila
kutetereka.
Pia tumenunua simu kuwa na tigo
pesa/m-pesa kupokea michango ya X-JKMs
- UKARABATI WA OFISI ZA JKM: Tunaangalia uwezekano wa kufanya
ukarabati mkubwa wa ofisi za JKM wakati wa likizo. Gharama za ukarabati
kwa sehemu kubwa tunaweza pata ufadhili usiozidi millioni tano toka nje.
Mapendekezo ni kuweka sakafu ya
marumaru (Tiles)
Viti vya ofisini vikarabatiwe.
Sehemu za kuta ambazo ndani zimeliwa na mchwa.
Kurekebisha sehemu ya vigae vya paa
vilivyo vibovu.
Mchanganuo na contracta atafutwe mara tu mitihani ikimalizika.
- TAARIFA NA MIPANGO MBALIMBALI YA UTENDAJI WA KAMATI ZA JKM KWA
MWAKA UJAO:
Kila Kamati itatoa taarifa ya mipango yao kwa mwaka ujao; ikiwamo pamoja
na mabadiliko ambayo zimependekeza kufanya. Kikao kitatoa ushauri,
kupendekeza mabadiliko yoyote kama yapo na kupitisha.
- Hali ya Imani/Uhai katika matawi. Nafasi kwa wajumbe kutoa maoni, taarifa
na namna ya kuboresha changamoto mbalimbali na kiimani na kimaadili zilizopo
katika matawi yetu na mahala tunapoishi na kupendekeza utatuzi wake.
- Tathmini ya utendaji na uendeshaji wa JKM. Ni fursa kwa wajumbe kutoa
maoni, kuhoji na kushauri juu ya mfumo na hali ya uendeshaji wa shughuli
mbalimbali za JKM katika hali zote; uongozi, fedha, chaguzi, sala n.k.
- MENGINEYO.
Toka kwa wajumbe na viongozi wengine.
Wajumbe ni viongozi wa
JKM, Matawi, Kamati ngazi zote pamoja na viongozi wa madarasa. Unakumbushwa
kuwahi ili kuanza na kumaliza kwa wakati.
Wako katika Kristo,
Alphonce M.K.M Nyalali
M/kiti
mdogo
0 comments:
Post a Comment