• A boat with beautiful sunset.
  • JKM GET TOGETHER
  • Amaizing sunrise moment

JKM RE-UNION


 

Ikiwa inatimia miaka 35 tangu kuanzishwa Jumuiya Katoliki Muhimbili, wanajumuiya waanakuomba ushiriki nao Jumapili ya tarehe 30 Machi, 2014 katika shughuli zifuatzo:

A)Misa maalum kwa ajili ya:

  1. Shukrani kwa Mungu kwa ajili ya Mapadre waanzilishi na walezi wengine wa jumuiya ( Fr. Joannet’, Fr. Lyampawe, Fr. Ngirwa, Fr. Mike na Fr.Mushi)
  2. Shukrani maalum kwa ajili ya wanajumuiya waliopita chuoni Muhimbili kama wanafunzi au wafanyakazi.
  3. Kmshukuru Mungu kwa uhai wa jumuiya na kukua hadi kuwa parokia mwaka 2008.
  4. Kuwaombea marehemu (1) waliowahi kuwa wanaJKM, (2) Fr. Lyampawe na (3) marehemu wazazi wa wanaJKM wa zamani na wa sasa.

B)Kuona shughuli na maendeleo/hali halisi ya jumuiya/kanisa la Muhimbili kwa sasa

C)Hafla fupi, maalum kwa ajili ya kuwakutanisha wanajkm wa miaka ya nyuma pamoja  na kupendekeza, kupitisha na kuzindua rasmi “program shirikishi”.

NB:

·         Misa itafanyika katika kanisa la Muhimbili kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 5:00. Pia Sadaka katika misa hiyo itaingia katika mfuko wa kutegemeza  shughuli mbalimbali za jumuiya.

·         Hafla itafanyika kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 8:30 mchana katika ukumbi uliopo ndani ya Parokia ya Immakulata, Upanga ambayo pia ni parokia mama wa Jumuiya Katoliki Muhimbili.

·         Taarifa za kiutendaji za miaka walau mitatu kurudi nyuma zitatumwa kwa barua pepe kwa wanajumuiya wote hasa wale watakaoshiriki ili wapate mda wa kusoma na kujua kinachoendelea katika jumuiya yao kwa sasa. Pia zitapatikana kwenye website ya jumuiya: www.jkmmcc.blogspot

·         Kama unamfahamu mwanajkm marehemu au kwa waliofiwa na wazazi wetu, tunakuomba ututumie majina yao kabla ya siku husika kwenye namba 0684163317 au email: alphonce.nyalali@gmail.com

·          “Program shirikishi” ni malengo yatakayowekwa yenye dhamira ya kuhakikisha uimara wa jumuiya hapa chuoni ambayo ni chombo muhimu cha malezi ya kiroho na kijamii kwa vijana waliopo chuoni. Pia inajumuisha shughuli zinazoweza kufanywa baina ya wanajumuiya waliomaliza, huko katika maeneo yao ya kazi pamoja na kudumisha ushirikiano baina yao huko waliko.

·         Tunaomba kwa wote watakaoshiriki wathibitishe kwa simu  0684163317 au email: alphonce.nyalali@gmail.com ili tuweze kufanya maandalizi yanayohitajika. Pia kama unamapendekezo zaidi kwa ajili ya siku hiyo tutafurahi sana ukitushirikisha.

 
Tunatanguliza shukrani kwa utayari na ushiriki wako.
 
Wenu katika Kristo,


Alphonce M.K Mashaka                                          Pd. Fidelis Safari Mushi

M/kiti Mdogo JKM                                                   Paroko na Padre Mlezi JKM

Simu: 0684 163317
           0655 163316
 
 
 
 
 

SHARE ON:

Hello guys, I'm Tien Tran, a freelance web designer and Wordpress nerd. Sed ut perspiciatis unde omnis iste natus error sit voluptatem accusantium doloremque laudantium, totam rem aperiam, eaque ipsa quae.

4 comments:

  1. Daima Mungu awenasi jumuiya ya JKM,azidi kuipa nguvu maana inatengenaza kizazi cha baadaye ,ni nani kati yetu anaweza ishi bila hekima ya Mungu

    ReplyDelete
  2. Mama Bikira Maria yu pamoja nasi daima kutuombea,this so good

    ReplyDelete
  3. Kwa Hakka nimda mfupi nimejiunga na JKM lakini maisha Yangu ya kiroho yamebadirika sana,nilikuwa nimezama kwenye matope na kufunikwa na wimbi la kubwa la kuangaishwa na madhehebu lakini Mungu kupitia JKM tazama kaninyamazisha kanitendea makubwa hata siwezi kusimulia.JAMENI NJOO MUONE MUNGU ALICHONITENDEA KUPITIA JKM,natamani niandike mengi lakini siwezi kuyamaliza.FR MUSHI TAZAMA MUNGU ANAVYO KUTAZAMA KUTOKA JUU NA KUKUBALIKI,upendo Mungu Baba na Mwana na Roho Mtakatifu uwe nawe JKM......Amen

    ReplyDelete
    Replies
    1. Amen,May the Lord enlighten your life to see his goodness and to save others

      Delete