Home
Archive for
May 2013
SHEREHE YA UZINDUZI WA TAWI LA UUGUZI CHINI YA MTAKATIFU AGATHA-19/05
Wanajumuiya wa mt Agatha wakiwa wanasikiliza kwa makini kinachoendele kwenye sherehe hiyo |
Baathi ya wageni waalikwa wakiwa wanatumbuizwa na bwana MC.Wageni hao walikuwa kutoka Jumuiya nyingine na Kwaya za JKM |
wanajumuiya wakiwa wanakula chakula cha sherehe |
wageni wakipata chochote |
HISTORIA FUPI YA JUMUIYA
Tumsifu yesu kristo.
Ifuatayo ni historia fupi ya
jumuiya.
Jumuiya
ya Uuguzi ilianza rasmi mwaka 2008 mara tu baada ya kufunguliwa kwa Parokia ya
Bikira Maria Salama ya wagonjwa Muhimbili wanaishi Jumuiya yetu ilifahamika kwa
jina la jumuiya ya Wauguzi.
Baada ya
Parokia kukua na kwa kutambua umuhimu wa Jumuiya katika parokia uongozi wa
Jumuiya Katoliki Muhimbili (JKM) kwa kushirikiana na Kamati tendaji ya
Parokia,ilipendekeza Jumuiya zote zipewe majina ya Watakatifu ambao pia
watakuwa wasimamizi wa jumuiya hizo
Mnamo
mwishoni mwa mwaka 2011,jumuiya zote zilipewa majina yaliyochaguliwa na
wanajumuiya wenyewe.Majina haya yalianza kutumika mwanzoni mwa mwaka 2012.Sisi
wanajumuiya wa tawi la Uuguzi tulioendekeza Jumuiya yetu iitwe Jumuiya ya
Mt,Agatha ambaye kanisa limemuweka kuwa msimamizi wa Wauuguzi wote.
Na leo hii tar
19/5/2013 Jumuiya hii imesimikwa rasmi na baba Paroko Pd.F Mushi kwa hiyo tangu
leo jukuiya hii itafahamika rasmi kwa jina la Jumuiya ya MT AGATHAilisomwa na mwenyekiti wa tawi.
SEMINA ELEKEZI YA VIONGOZI -MBAGALA
Safari ilianza toka Chole na Muhimbili saa 1:30asb na tukafika Mbagala kama kwenye saa mbili na nusu hv.
Bahadhi ya washiriki wakiwa wamewasili kwenye eneo la tukio |
Wanaume wa kazi nao waliweza kuatendi hiyo semina |
Baada ya kuwasili registration ya wote waliohudhuria hiyo semina ilianza na baada ya hapo tukaingia ukumbi kwa ajiri ya kufungua semina yetu
walengwa wa semina wakijiandikisha majina yao |
Baba paroko father Mushi alitufungulia semina kwa sala na kutoa maneno yake ya ufunguzi
Mwenyekiti wa JKM akatoa taarifa kuhusu uwendeshaji wa JKM kwa mwaka uliopita
Baada ya hapo ikawa asubuhi ikawa teabreak.
Baada ya teabreak ilifuata somo la kwanza ambalo lilitolewa na brother Chotta(MD5)
sifa za kiongozi bora ni kuwa Mtumishi wa watu,Mchungaji wa watu na kiongozi ni wakili wa yesu |
Semina ikiendelea..
Bahadhi ya michezo ndani ya semina ilikuchangamshana kidogo
Baada ya hapo ikafuata kipindi cha pili kikaanza
lunch ilikuwa kama hivi
makabithiano ya uongozi katika ngazi zote za JKM
Nahawa ndio wenyeviti wa JKM 2013/14
kutoka kushoto Suzana(mkiti 1),Alfonce(mwenyekiti) and Benard(mkiti 2) |
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)