JE ULIYAKOSA MAFUNDISHO YAKE KAKA NAZARETH MWEMA SIKU YA SEMINA YA VIONGOZI WA JUMUIYA?
Mtu wangu popote ulipo kama uliikosa hii hotuba yake Kaka Nazareth ambaye ni Mwenyekiti mtaafu wa Jumuiya ya Wat COSMA & DAMIANO, aliyoitoa siku ya SEMINA YA VIONGOZI pale Mbagala Spiritual Centre, siku ya tarehe 21 May, 2016, JKM inakusogezea taarifa kamili hapa chini.. KAKA MWEMA aliyasema haya <<<<<< click here to view more>>>>>
PAROKIA YA BIKIRA MARIA SALAMA YA WAGONJWA
JUMUIYA KATOLIKI YA MUHIMBILI
*************************************************
SEMINA YA VIONGOZI WA JUMUIYA.
MBAGALA SPIRITUAL CENTRE. 21st May, 2016.
*********************************************
YALIYOMO.
1. Utangulizi
2. Maana ya uongozi
3. Tofauti ya kiongozi wa Kikundi cha dini na wa Kidunia
4. Wajibu wa jumla wa Kiongozi wa Kidini.
5. Changamoto za Kiongozi/Uongozi.
6. Mafao (Thawabu) za Uongozi.
7. Hitimisho
1.UTANGULIZI.
Popote unapoona kazi ya Mungu imesonga mbele na kufanya vizuri
lazima kuna kiongozi aliyesimama kwenye nafasi yake vizuri. Imekuwa ni
tabia ya Mungu mara zote kumchagua mtu ili kuyafanikisha malengo na
mipango yake.
MIFANO :
**Mungu alimuandaa Ibrahimu - Mwanzo 12: 1-2;
**Akamwandaa Musa ili kuwatoa waisrael Utumwani - Kut.3:2-14.
**Mungu alitumia wanaume na wanawake katika kufikia malengo
yake kama vile Nabii Debora - Waamuzi 4:4. Na mama Bikira Maria.
2.MAANA YA KIONGOZI /UONGOZI
**Uongozi ni hali/tendo la kuongoza.
Ni hali ya kutangulia mbele, kusimamia, kulinda na kuelekeza
watu njia au mwelekeo wa kuuendea au kufikia malengo Fulani.
**Kiongozi wa kidini ni mtu aliyepewa dhamana (aliyeaminiwa)
na Mungu kuongoza watu wengine (kuwatumikia). Mfano:
Musa,Yona –
**Uongozi ni karama ya kuonyesha njia kwa vitendo.
kiongozi bora si mtu wa kulalamika bali anatafuta ufumbuzi wa
changamoto za kundi analoliongoza na hivyo akiongea, watu
husikiliza.
3. TOFAUTI KATI YA UONGOZI WA KIDINI NA WA KIDUNIA.
i) Hitaji na namna ya kumuandaa Kiongozi.
Mungu huandaa na kumweka Kiongozi. 1Sam.16:3,7 Ezek.16:1 - 5,
1Tim.3:1,15 Yer.3:15 Math.9:38.
ii) Nia ya ndani ya Kiongozi.
Mtu anaweza kuwa kiongozi kwa nia ya kutaka kuyafanya mapenzi ya
Mungu. FIlipi.2:5, 13. Zipo nia mbalimbali pia kama vile kutaka:- mamlaka,
sifa, kuheshimiwa, utukufu, kutambulika, kiburi n.k.
*Hizo ni nia za Kiongozi wa Kidunia*
Kumbuka:
Uongozi wa kidunia unadhihirishwa katika nia binafsi katika kupata mafao
yenye kumnufaisha yeye, kupata marupurupu mazuri mfano, heshima;
Mungu anasema “Msitende neno lolote kwa kushindana wala majivuno, bali
kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi
yake. Fip.2:3 - 4.
iii) Kutaka mapenzi ya Mungu.
Rum.12:2, Efe.5:17, 1Tim.3:1
Nia yake ya moyoni ndiyo itakayobainisha kama atakuwa wa Kiroho au wa
Kidunia.
4.WAJIBU WA JUMLA WA KIONGOZI WA KIDINI
Yhn 10:11 – 15.
Wajibu ni majukumu (kazi) apaswayo kiongozi kuyafanya kwa nguvu zake
zote ili kuyatimiza malengo yake. Tukigawa katika sehemu mbili kuu:
I} KULITUNZA KUNDI
Ni wajibu wa kiongozi kulilinda, kulichunga na kulihakikishia usalama kundi
analoliongoza dhidi ya Mbwamwitu wakali:waharibifu na wazushi ambao
jumuiya siyo wito wao pia dhidi ya Imani potofu: Mafundisho ya uongo au
yaliyo kinyume na kanisa Katoliki la Roma.
Kumbuka:
watu wa Mungu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa, Elimu sahihi ya neno
la Mungu. Hosea 4:6, Hali kadhalika wanapona kwa maarifa. Mith 11:9,
II} KUJITUNZA NAFSI YAKE
Nafsi imebeba:- Akili ,Makusudi (nia),Hisia, 1Kor 15:33 – 34
Hivyo kama kiongozi lazima uitawale nafsi yako mbele ya hao
unaowaongoza. Ni lazima ujiepushe na yale yanayoweza kuharibu sifa yako
kama kiongozi wa kundi.
Sifa za viongozi wa kidini ambao hufanikiwa.
i) Wana maono yaliyo wazi.
ii) Hujiwekea mipango na ratiba ya kutimiza maono hayo.
iii) Wanashirikiana na viongozi wengine. Mawasiliano ni muhimu.
vi) Huvumilia wakati maono, malengo na mipango inapokutana na
vikwazo mbalimbali na kutotimiza malengo aliyokusudia.
v) Hupata ufumbuzi na kubuni njia ya kuendelea mbele si kurudi nyuma na kukata tamaa.
vi) Kujitoa kwa Kristo (Bwana – Mungu) – 2Kor 8:5 16
vii) Utii. mwz. 12:1 – 4
viii) Uaminifu: 1kor. 4:1 – 2. Kipimo cha Kiongozi. Uaminifu
Katika Maagano, Mahudhurio na Kujali Muda.
ix) Tabia na nidhamu kadiri ya mafundisho ya dini: Mdo 6:4 .
x) Uwajibikaji: Mark 6:7, 30:-
5.CHANGAMOTO ZA UONGOZI.
Yoh. 10:11, Lk. 15:4, 1Sam. 17:35 - 37.
**Kujitoa muhanga kwa ajili ya wengine - (Personal sacrifice)
**Mateso ya kibinafsi - Kutokana na hisia mbalimbali.
**Kukataliwa, kukatishwa tamaa, kulaumiwa, kudhalilishwa.
**kutengana kimajukumu. Mfano kukosa muda wa kuangalia mpira.
**kusingiziwa, upweke, shutuma, chuki,kusemwa.,kuudhiwa.
**Kuingiliwa katika maisha kwa mambo binafsi.
6.THAWABU ZA UONGOZI.
Thes. 5:12 - 13, Ebr. 13:17, 1Petr. 5:2 - 4, 1Kor. 9:10.
Heshima katika jamii - (Social Status)
Kutambuliwa na kueleweka kwa karama zilizopo ndani yako
Mafao ya Kiroho (Spiritual Benefits) kujiongezea imani.
Taji ya utukufu (Glorious Crown) Dan. 12:3 na 1Kor. 15:41.
Kupata kibali kwa Mungu na kwa wanadamu (God’s favour) - Mith. 3:3 – 4.
7.HITIMISHO.
Viongozi mjue kuwa umeaminiwa katika nafasi zenu. Mwisho wa uongozi
wenu mtatakiwa kujitathmin kwa yale mliyofanya. Na sasa mjiulize maswali
haya.
1.Je, Kiongozi anahitajika katika nafasi yako uliyoaminiwa?
2.kuna tofauti kati ya Uongozi na Utawala.Je, Wewe ni kiongozi au
Mtawala?
3.Utafanya nini wewe binafsi ili kuboresha uongozi wako?
4.Tukigawa viongozi katika makundi mawili: Wale wanasababisha
mambo mazuri kutokea na Wale wanaosubiri mambo yatokee
yaliyofanywa na wengine. Je umejiandaa kuwa aina ipi ya kiongozi?
5. katika uongozi kuna changamoto mbalimbali, je umejiandaa
kuvumilia mpaka mwisho kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
“Tunawatakieni mafanikio na uongozi mwema. Mungu mwenyewe na
akawaongoze kuifanya kazi yake.”
************ ASANTENI***********
Presented by.
Nazareth Mbilinyi