• A boat with beautiful sunset.
  • JKM GET TOGETHER
  • Amaizing sunrise moment

SEMINA YA VIONGOZI ILIYOAMBATANA NA MAKABIDHIANO YA UONGOZI KWA VIONGOZI WAPYA ILIYOFANYIKA MBAGALA SPIRITUAL CENTRE TAREHE 09/05/2015

Ukiwa ni muda wa mapumziko, hapo ndio viongozi wanapata kubadilishana machache,kufahamiana n.k yote huchanganywa pamoja.

Kumbe hata kutembea wana JKM hushirikiana!!! Kweli yatupasa kufanya mambo mengi kwa upendo na umoja. Usimuache mwana JKM mwenzako nyuma, twende pamoja katika hii safari.

Mwenyekiti mpya akibadilishana mawili matatu na baadhi ya viongozi wake, mfano mzuri pia.

Huo muda hatuulizi kama unazembea,.. maana ukizembea hapo huku boom linakata hahahaha, utamrudia Mgaya.

Hapo Bruda wa nadhili fupi fupi akiwashirikisha viongozi, sijui nao wanavutiwa ama anawaelekeza namna ya kuwa na nadhili intermittent.

Naona hapa hamna anaemwongelesha mwenzake, kazi tu.

Ukianza ku-skip halafu ukaiona hii picha na wewe u mmoja wao, nahisi utaishia kupiga miayo.

Haya katibu na camera man anakuangalia ka unavofanya wewe.

Mmmmmh, kuwa JKM kuna raha nyingi, hapo nahisi stress zote za MUHAS zinapotea, isipokuwa kwa ndugu yangu Katto maana anaonekana sijui anawaza Davidson's Clinical medicine au Internal medicine.

Ati baada ya kupiga picha camera man akaanza kuwaza, ''mbona Mr. Rumende ana sura ya ualimu na anapendeza akiwa mwalimu'' hahaha. Camera man nae bhana.

Hongera mmependeza viongozi.

Wakiwa na furaha huku wakiendelea na kilichowakalisha mezani.

Wenyewe walikuwa wanasema Table ya mwisho na ya upendeleo, Hebu ngoja tuwaone kweli.

Duuuuh, kumbe kweli ni ya upendeleo, naona wanaongezewa tu na wakiwa na furaha

Mtoa maada a.k.a Jembe ka alivoitwa kwa siku hiyo, Stella Mwinuka akiendelea na maada na pembeni M/kiti mstaafu Kweyamba nae akifuatilia kwa makini.Tutakumiss sana dada Stella.
.
Wakiendelea kufuatilia maada kwa makini. Na kweli jitahidini mkayaishi na kuyatumia mlosikia toka kwa dada na yote mliyoyaandika kama kumbukumbu.

Kiongozi akionesha mfano mzuri wa uchukuaji notes na umuhimu wa kumbukumbu. Safi sana ,ila uyatumie kweli uloandika.

Wakiwa wanaandaa kishirikisho cha mchezo ni kaka Kazaura na dada Asteria, tutakumiss sana kaka Kazaura kwa ubunifu wako mwingi.

Maada ikiendelea.

Wakiendelea kufuatilia kwa umakini.

What an exception talk from our sister Stella Mwinuka!!! Mungu akubariki zaidi dada.

Wakiwa na kopi za maada na wakifuatilia kila kipengele.

Finalists haoooo!!! Jamani tutawamiss, tunatamani muendelee kubaki ama mrudi kuajiliwa karibu na Muhas kama vile MNH na Tumaini. Ila si kama tutakavyo sisi, bali kama location ya wagonjwa wengi wanaohitaji msaada wenu inavyosomeka.

Mungu awafanye muwe viongozi bora na wabunifu.


Hapa naona hamna anaeachwa kumbe.


Dada Stella akiwa anahitimisha maada yake.

Wakiwa wenye tabasamu, inaonekana wanaelewa zaidi.

Haya sasa, mambo ya Bruda wa nadhili za muda ndo yanaanza.

Hapo somo la kushirikiana katika kuwafikisha kondoo kwa bwana wao ndo linaeleweka zaidi na huo mchezo.

Timu B ya M/kiti kaka Antimoni iko tayari .

Finalist hao wakiwepo na waibiaji wa picha wawili walio kwenye blu na kijani. Tutawakumbuka sana jamani akiwemo camera man, maana atakosa kuzipiga picha sura zenu. Mkawe wajumbe wazuri wa Kristu paka wodini.

Its called Stress free zone and moments.

Timu A ya kaka Kweyamba naona wamedhamiria kujaza kikopo toka umbali wa Mita 15 hivi alipo Captain wao. Hapo lazima akili itumike.

Kazana kaka naona waweza okoa timu yako.

Sasa sijui tuseme haya maji yanapitaje hapa, nahisi kaka atakuwa kama receptor's blocker.

Ama kweli mwihowe juhudi zimezaa matunda na Timu A ya kaka Kweyamba imeshinda. Hatutakiwi kukata tamaa kama viongozi bali kuvumilia na kuwa wabunifu ikiwemo kutumia kila mtu katika sehemu anayoweza zaidi a.k.a Strengths zake.

Marefa sasa wamepuriza filimbi ya mwisho na sample zinachukuliwa kupata matokeo.

Hahahaha, mashabiki nao bhana, wanafuraaahi. Kumbe furaha tunatakiwa kushare wote bila kujalisha nani kaleta ushindi.

Na mshindi kapatikana.

Camera man nae kumbe anapenda kuwa kwenye picha. Sikujua bhana.

Brothers in Christ.

Hapa sio ku-edit bali camera man aliipigia kwenye tundu akiwa nje. Its looking awesome anyway japo hakuna watu.

Lunch time inaitwa

Umoja unaendelezwa kotekote.

Haya Bruda naona kweli unadhihirisha neno la Yesu ''ukitaka kuwa mkubwa lazima uwe mtumishi wa wengine wote''. Hudumia kaka.

JKM ina kila aina ya watumishi wa Bwana.

Hapo ni wewe tu unajipakulia, nahisi hiyo itakufanya uisahau cafeteria ya Mgaya.

Picha kutokea nje, ilipigiwa kwenye tundu. Wanaonekana wakiendelea na kazi.

Kwa furaha na upendo wakiendelea kula na kujadili mawili matatu.

Kwa vitendo zaidi.

They call it adittion, so mbaya.

Wenyeviti wa matawi ya Chole,Vitivo,MTC na Uuguzi katika kuelekea makabidhiano. Kutoka kushoto M/kiti wa Chole, aliyekuwa M/kiti wa Vitivo,M/kiti wa MTC, na muwakilishi wa M/kiti wa Uuguzi.

Wawakilishi wa madarasa na Blocks toka jumuiya ya Mt. Fransisco wa Asizi, Chole wakijitambulisha.

Viongozi wa JKM  Chole.

Wakiwa na M/kiti wao na kukumbatiana kwa furaha.

Viongozi wa madarasa jumuiya ya Wat. Cosmas na Damiano.

Viongozi wa kamati tendaji, VITIVO.


Viongozi wa kamati kuu, Chole.

Viongozi wa Kwaya ya Mt. Augustino.

Mwenyekiti kaka Antimony(kushoto) na M/kiti msaidizi dada Angel (kushoto).

Picha ya pamoja

Picha ya pamoja ya wenyeviti wote na makatibu wote.

Picha ya pamoja ya viongozi wote.

When funny becomes funniest.

Captured by brother Alex Kamugisha.

Was the last photo, and as per camera man it was credited as the best photo of the day. Hongera dada, wanasema its a nice photo. Amaizing fulani hivi.

SHARE ON:

Hello guys, I'm Tien Tran, a freelance web designer and Wordpress nerd. Sed ut perspiciatis unde omnis iste natus error sit voluptatem accusantium doloremque laudantium, totam rem aperiam, eaque ipsa quae.

2 comments: