• A boat with beautiful sunset.
  • JKM GET TOGETHER
  • Amaizing sunrise moment

TOPIC:ABORTION,..By ASTERIA JULIUS THAT WAS DONE ON TUESDAY 23/June/2015 FOR COSMAS AND DAMIAN COMMUNITY

Abortion is among most headaches to many people of different carriers,politicians,lawyers,medical professionals,individuals and many more. Asteria has prepared a best and simple presentation by which everyone can do self assessment on how oneself is the causative and can also be of help in prevention of it.

UHAI……. Zawadi ya Mungu, mali ya Mungu

WACHANGIAJI WA JANGA LA UTOAJI MIMBA
o   Je umejaribu kutafakari jinsi wewe na mimi tunavyochangia ?

o   Je wewe na mimi hatujakaa kimya hali tukiona vitendo vya utoaji mimba vikifanyika ?
o   Je tumewahi kukemea vitendo hivyo hadharani watu wakasikia ?
o   Je tumewahi kumkabili mtoaji mimba mwenyewe tukamwambia kuwa amefanya makosa kumuua motto wake?
o   Je tumewahi kuchukua hatua za kisheria dhidi ya yeyote alietoa mimba ?
o   Je wewe na mimi hatujatoa fedha kumsaidia rafiki yetu/ mshikaji wetu kutoa mimba?
o   Je hatujamsindikiza au kumpeleka rafiki zetu/ mke kwa maganga kutoa mimba ?
1.       Daktari/ nesi/ mtoaji dawa
o   Huyu amechangia moja kwa moja katika kuua: huyu ndiye muuaji
o   Ni yeye ameniaminisha kuwa utoaji mimba ni kitendo cha kawaida tu tena cha mara moja kisichokuwa na madhara yoyote : maumivu
o   Huyu ndie anayedanganya kuwa aliemo tumboni sio mototo, si binadamu, ni nyama tu, ni damu damu tu sawa na damu ya mwezi
o   Pia anawaeleza aliemo tumboni ni kiumbe tu chenye kichwa kikubwa na mkia mdogo
o   Utoaji mimba ni jambo la biashara huwaingizia kipato kikubwa.
2.       Mama wa mototo
o   Mama anafanya uamuzi ( uwe wa hiari au kulazimishwa) ndie anayemwambia mganga/ daktari  muue mtoto huyu simtaki
o   Ili mama aue mtoto wake lazima atumie uongo na visingivio mfano:
maisha yangu ni magumu, sina fedha
baba wa mtoto amenitelekeza
3.       Baba wa mtoto
o   anaweza kushiriki moja kwa moja kutoa fedha za kumuua mtoto, kumsindikiza
anaweza kuwa amekataa na/ au kutekeleza mimba hiyo kwa kuogopa malezi yap eke yake mama anaweza kulazimika, kama njia ya kumkomboa baba wa mtoto huyo
4.       Ndugu marafiki huchangia kwa
o   kumzomea mwenzao kwa kupata mimba akiwa mwanafunzi, mke au mshikaji wa mtu mwingine , bado ananyonyesha, umri mdogo au mkubwa
5.     Bunge
          o   kutunga sheria zinazoruhusu utoaji mimba
o   kushindwa kutunga sheria za kuwalinda binadamu dhaifu
o   kusikiliza hoja za watetezi wa vifo bila kuzifanyia ufumbuzi wa kina
6.       mahakama
o   kushindwa kutoa hukumu zinazowalinda watoto
o   kupindisha tafsiri ya sheria ili itumikie maslahi ya watetezi wa vifo
o   kushindwa kutoa adhabu kalipale ambapo utoaji mimba hauruhusiwi


7.       mashirika mabalimbali
o   kuhamasisha kupitia kampeni na program kwaajili ya utoaji mimba
o   kuziteka mamlaka na taasis za serikali kwa udanganyifu wa fedha nyingi
o   kutumia lugha inayomdunisha binadamu aliye tumboni ili aonekane kuwa sio mtu
o   katika kuweka na kutekeleza sheria/kanuni/taratibu za kuwafukuza wanawake wapatapo mimba
o   ajira zinazombagua mwanamke mjamzito
o   mtazamo wa kumwona mwanamke mjamzito kama ni mzinzi mkubwa hasa katika taasisi za kidini.
8.       Wanasayansi hasa wale waliosomea elimu juu ya mimba.
o   Kuchagua mtoto wa jinsi wanayotaka
o   Watoto wanaobainika kuwa na ulemavu
9.       Viongozi wa dini
o   Hushiriki kutokana na ukimya wao ambapo huwafanya waamini wabaki njia panda.
o   Hujiuliza je utoaji mimba ni dhambi mbele ya Mungu ? mbona viongozi wetu hawasemi lolote

Wajibu wetu
Kwa kuwa karibia wote tunahusika kwa namna moja au nyingine katika janga hili la utoaji
mimba. Wajibu wetu ni kulitokomeza kwa kufanya hivi.
ü  Kuwa mashahidi sisi wenyewe
ü  Kutofumbia macho uovu huu
ü  Kuufichua ukweli
ü  Kuandika, kuongea na kutumia vyombo vya habari kutetea uhai kusali na kuombea watu wabadilike

Imeandaliwa na kuletwa kwenu  nami Asteria Julius,




SHARE ON:

Hello guys, I'm Tien Tran, a freelance web designer and Wordpress nerd. Sed ut perspiciatis unde omnis iste natus error sit voluptatem accusantium doloremque laudantium, totam rem aperiam, eaque ipsa quae.

1 comments:

  1. What a good personal evaluative words,... wish everyone could read and do his/her responsibility on stoping this.

    ReplyDelete