• A boat with beautiful sunset.
  • JKM GET TOGETHER
  • Amaizing sunrise moment

AGENDA ZA KIKAO CHA HALMASHAULI 6/07 Saa 2:00asbh-5:3asbh


JUMUIYA KATOLIKI MUHIMBILI
KIKAO CHA HALMASHAURI YA JKM, JUMAMOSI TRH 06/07/2013
 saa2:00asbh – 5:30asbh
AGENDA ZA KIKAO

  1. MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI  2013/2014: Rejea pendekezo la bajeti lililoambatanishwa. Kikao kitajadili, kurekebisha na kupitisha  makadirio hayo.( nakala za bajeti.zipo kwa wenyeviti wa matawi na viongozi jkm, ubao wa matangazo ofisini, facebook na www.jkmmcc.blogspot)
  2. JKM GRAND FUND RAISING:
*    Bahasha na fomu kwa wakatoliki wote wanaosoma MUHAS.
*    Fomu zitakuwa ndani ya kila bahasha na tunapendekeza watu wapitishe fomu kwa ndugu na jamaa zao wakati wa likizo.
*    Hatulazimishi mtu kutembeza fomu, ia kini walau kila fomu na bahasha yake irudi na kima cha chini ambacho mapendekezo ni Tsh 10000 ( elfu kumi za kitanzania). Tunapendekeza watu watoe zaidi ili kupata fedha ya kutosha kuendesha hadi mwaka 2015 au zaidi bila kutetereka.
*    Pia tumenunua simu kuwa na tigo pesa/m-pesa kupokea michango ya X-JKMs
  1. UKARABATI WA OFISI ZA JKM: Tunaangalia uwezekano wa kufanya ukarabati mkubwa wa ofisi za JKM wakati wa likizo. Gharama za ukarabati kwa sehemu kubwa tunaweza pata ufadhili usiozidi millioni tano toka nje.
*    Mapendekezo ni kuweka sakafu ya marumaru (Tiles)
*    Viti vya ofisini vikarabatiwe.
*    Sehemu za kuta ambazo ndani  zimeliwa na mchwa.
*    Kurekebisha sehemu ya vigae vya paa vilivyo vibovu.
Mchanganuo na contracta atafutwe mara tu mitihani ikimalizika.

  1. TAARIFA NA MIPANGO MBALIMBALI YA UTENDAJI WA KAMATI ZA JKM KWA MWAKA UJAO: Kila Kamati itatoa taarifa ya mipango yao kwa mwaka ujao; ikiwamo pamoja na mabadiliko ambayo zimependekeza kufanya. Kikao kitatoa ushauri, kupendekeza mabadiliko yoyote kama yapo na kupitisha.
  2. Hali ya Imani/Uhai katika matawi. Nafasi kwa wajumbe kutoa maoni, taarifa na namna ya kuboresha changamoto mbalimbali na kiimani na kimaadili zilizopo katika matawi yetu na mahala tunapoishi na kupendekeza utatuzi wake.
  3. Tathmini ya utendaji na uendeshaji wa JKM. Ni fursa kwa wajumbe kutoa maoni, kuhoji na kushauri juu ya mfumo na hali ya uendeshaji wa shughuli mbalimbali za JKM katika hali zote; uongozi, fedha, chaguzi, sala n.k.
  4. MENGINEYO. Toka kwa wajumbe na viongozi wengine.

Wajumbe ni viongozi wa JKM, Matawi, Kamati ngazi zote pamoja na viongozi wa madarasa. Unakumbushwa kuwahi ili kuanza na kumaliza kwa wakati.
Wako katika Kristo,
                              Alphonce M.K.M Nyalali
                              M/kiti mdogo

SHARE ON:

Hello guys, I'm Tien Tran, a freelance web designer and Wordpress nerd. Sed ut perspiciatis unde omnis iste natus error sit voluptatem accusantium doloremque laudantium, totam rem aperiam, eaque ipsa quae.

    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment